Azam FC hiyo nusu fainali , Yaitungua Simba 1 – 0…..


Mabngwa watetezi wa kombe la mapinduzi , Azam FC wameonyesha nia yako ya kutetea taji hilo baada ya kutinga hatua ya nusu fainali kwa kuifunga Klabu ya Simba goli 1-0 katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea kisiwani Zanzibar .

Goli pekee la mchezo lilitupiwa wavuni na Iddi Kipwagile  dakika ya 59  baada ya kumalizia  pasi ya kiungo Frank Domayo .

Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi tisa ikikamilisha mechi zake nne za Kundi A kwa ushindi wa mechi tatu na kufungwa moja na URA ya Uganda.
Simba inabaki na pointi zake nne baada ya mechi tatu, ikishinda moja na sare moja na itaingia kwenye mchezo wake wa mwisho na URA Jumatatu kusaka lazima ushindi ili kwenda Nusu Fainali.
Mchezo uliotangulia wa Kundi B, Singida United iliibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya JKU mabao ya Daniel Lyanga dakika ya 19 na Elinywesia Sumbi dakika ya 20.
Singida United wanafikisha pointi 12 baada ya mechi zao nne na watakamilisha mechi zao za Kundi B kwa kumenyana na Yanga SC inayoshika nafasi ya pili kwa pointi zake tisa Jumatatu. Singida na Yanga zimekwishafuzu Nusu Fainali.

 

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com