Azam TV Kuonyesha Live mechi ya Taifa Stars vs Algeria leo…


Leo timu ya taifa ya Algeria itaikaribisha Taifa Stars katika mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Mustapha Tchaker kuanzia saa 1:00 usiku kwa saa za huko sawa na saa 3:00 usiku saa za Tanzania mjini Bilda. Starts watakuwa ugenini kuwakabili Algeria katika mchezo wa marudiano uliobeba taswira ya miujiza kwa Stars kupata ushindi kwenye Uwanja wa Mustapha Tchaker saa tatu usiku kwa saa za Tanzania.

 azam-live-Taifa-Stars-vs-Algeria-Bongosoka
Ili kuwaondoa Algeria nyumbani kwao, Taifa Stars yenye matumaini kibao ya kushinda mechi hiyo, inahitaji ushindi wa aina yoyote au sare ya 3-3, kinyume chake itakosa kucheza hatua ya makundi kwa safari ya Russia, hivyo kusubiri safari nyingine kama hiyo, Qatar mwaka 2022..
Taifa Stars ilikaribia kuandika rekodi ya ubabe mbele ya Waarabu hao baada ya kuongoza kwa mabao 2-0 hadi dakika ya 70 waliporuhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya 2-2.
Akizungumza kwa simu na Nipashe, Kocha Boniface alisema hakutakuwa tena na makosa ya kiufundi kutoka kwake kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa Dar es Salaam.  Mkwasa amesema kuwa kikosi chake kitacheza soka la kushambulia na kulinda goli kwa umakini zaidi ya mchezo wa kwanza.
“Nimewaambia wachezaji wangu, mchezo wa leo ni mgumu kwetu kwa mazingira ya ndani na nje ya uwanja,” alisema Mkwasa. “Tunahitaji kufunga mabao ya mapema ili kuwaweka kwenye wakati mgumu, tusiruhusu mashambulizi. Tunaweza kupata ushindi ugenini” Mkwasa aliongeza.
Naye Mshambuliaji tegemeo wa Stars, Mbwana Samatta, alisema kwamba mechi hiyo inatarajiwa kuwa ngumu na wamejipanga kucheza kwa kasi zaidi ya ile waliyoionyesha Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Samatta alisema kwamba hawajakata tamaa ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo na lolote linaweza kutokea kwenye soka huku akisisitiza kuwa dakika 90 zilizobakia leo ndiyo zitaamua mshindi.
“Tumekuja kupambana, tumekuja kurekebisha makosa tuliyofanya katika mchezo wa kwanza, tutakuwa makini zaidi kwa sababu hii ndiyo nafasi yetu ya mwisho,” alisema Samatta anayecheza soka la kulipwa na klabu ya Klabu Bingwa Afrika, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).
 “Mchezo utakuwa mgumu, lakini tunahitaji kucheza kwa nidhamu kubwa ili kuepuka kuwa sababu ya wapinzani wetu kupata ushindi.”
 Mechi ya leo kati ya Taifa Stars dhidi ya Algeria itarushwa moja kwa moja na channel zilizo katika kingamuzi cha Azam ingawa bado haijajulikana ni channel gani .

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com