Azam VS Gor Mahia , fainali ya kihistoria Kagame Cup..


AZAM FC  na Gor Mahia zitacheza Fainali ya Kagame Cup, Kombe la Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na ya Kati, leo ,  Jumapili Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam. Azam hadi sasa ina rekodi  ya kucheza kwa dakika 450 bila kuruhusu bao lolote na kumfanya kipa Aishi Manula na safu yake ya ulinzi kujiandikia rekodi nyingine ya kutofungwa mchezo kati ya tano kuanzia hatua ya makundi. Ukiachana na rekodi ya Azam ya kutokupoteza mchezo ukiangalia upande wa pili  Gor Mahia  pia inashikilia rekodi ya kucheza mechi mfululizo mwaka huu bila kupoteza, ikiwa imefikisha 24, zikiwamo 18 za Ligi Kuu Kenya wanayoiongoza na sita za Kombe la Kagame.

Azam-Gor-Mahia-fainali-CECAFA-Kagame-Cup-bongosoka

Azam fc ya Tanzania inayonolewa na kocha Muingereza Stewart Hall aliyewahi kuifikisha fainali za Kagame mwaka 2012 na Gor Mahia iliyo chini ya kocha Mscotish, Frank Nuttal  zitakua na kibarua kigumu cha kuweka historia mbili tofauti ambapo kwa Gor Mahia watakua wakilisaka  taji la kwanza baada ya miaka 30  ambapo  ilifika fainali na kunyakua taji mwaka 1985  japokua  walishacheza fainali 7 mwaka 1976, 1977, 1980, 1981, 1984 na 1985 ambazo walichukua kombe fainali zote isipokua moja ya mwaka 1984. Kwa upande wa Azam , watakua wanakumbuka machungu ya mwaka 2012 , walipocheza fainali yao ya kwanza na kupoteza kwa kupigwa goli 2 – 0 na Yanga . Azam wanaingia uwanjani leo kusaka taji la kwanza la Kagame. Mbali na timu hizo kuwa katika vita ya kuwania rekodi mpya, pia kutakuwa na mchuano mkali wa kuwania Kiatu cha Dhahabu kati ya mastraika Michael Olunga wa Gor mwenye mabao matano na Kipre Tchetche wa Azam mwenye mabao matatu.

Kikosi cha Azam kinachotegemewa kuanza:  Aishi Salum Manula (GK), Aggrey Morris, Pascal Serge Wawa, Said Hussein Moradi, Shomari Kapombe, Farid Musa Malik Shah, Jean Baptiste Mugiraneza, Frank Raymond Domayo, Himid Mao, John Raphael Bocco (C) and Kipre Herman Tchetche.

Kikosi cha Gor Mahia kinachotegemewa kuanza: Boniface Oluoch (GK), Karim Nigiziyimana, Abouba Sibomana, Musa Muhammad (C), Haroun Shakava, Eric Ochieng, Aucho Khalid, Godfrey Walusimbi, Innocent Wafula, Meddie Kagere and Michael Olunga.

Mchezo huo wa fainali kati ya Azam fc na Gor Mahia utatanguliwa na mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baina ya Al Khartoum na KCCA ambao watavaana muda mchana.

 

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com