Breaking News : Kocha Simba ajiuzulu…


Kocha msaidizi wa klabu ya wekundu wa msimbazi , Jackson Mayanja ameamua kuachana na klabu hiyo na  kurejea nchini kwake Uganda.

Mayanja ambaye bado yuko jijini Dar es Salaam, ameamua kuachana na Simba akidai ana matatizo yake binafsi.

“Ni matatizo ya kifamilia lakini suala hilo siwezi kulizungumzia kwa sasa,” alisema.

Lakini habari kutoka Simba zimeeleza kuwa sasa wako katika hatua za mwisho kuvunja mkataba wake baada ya kukubaliana naye kutokana na uamuzi wake huo.

Hadi sasa simba imeshacheza michezo 6 huku ikiwa na pointi 12, ikiongoza msimamo wa ligi kuu kwa idadi ya magoli ya kufunga na kufungwa 11  huku Yanga na Mtibwa  wote wakiwa nyuma na pointi 12 na idadi sawa ya magoli (3)  pamoja na michezo.

 

 

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com