Elias Maguli njiani kutua Yanga


Bao la mshambuliaji Elius Maguli wakati akiitumikia timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ , limeonekana kuchagiza mchakato wa Klabu ya Yanga kukamilisha usajili wa nyota huyo kwa mabingwa hao wa soka nchini.

Maguli alifunga bao zuri kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, wakati Taifa Stars ilipocheza na Algeria katika mchezo wa kutafuta kupangwa katika makundi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Elias-Maguri-Stand-United-Taifa-Stars-Bongosoka

Licha ya mchezo huo kumalizika kwa sare ya mabao 2-2, lakini makocha wa Yanga, Hans van der Pluijm na msaidizi wake, Juma Mwambusi, waliokuwapo uwanjani hapo wakilazimika kufanya kazi ya ziada kumjadili mshambuliaji huyo wa Stand United ya Shinyanga.

Pluijm alionekana kuvutiwa na Maguli jinsi alivyocheza na hata alipofunga bao hilo kiufundi kwa kichwa dakika ya 42. Pluijm alishindwa kuvumilia na badala yake alimwita msaidizi wake Mwambusi na kujadili kwa dakika kadhaa.

Mwambusi anaelezwa kulipendekeza jina la Maguli katika ripoti yake kutokana na kazi maalumu aliyopewa na Pluijm ya kuangalia mikanda ya timu zote zilizocheza katika Ligi Kuu kabla haijasimama.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com