Hans Pluijm azipigia hesabu Simba , Yanga. Ataja mbinu zake….


Kocha mkuu wa klabu ya Singida United ,  Hans van Der Pluijm amekaririwa akisema  kua anazitamani timu za Simba na Yanga ili kuonyesha ubora wa kikosi chake.

Kocha Van Der Pluijm ambaye ni kocha wa zamani wa Yanga, amedai kuwa kikosi chake kimeimarika tofauti na ilivyokuwa kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu, ambapo amedai kuwa kipimo kizuri kwake hivi sasa ni kukutana na vigogo hao wa soka la Tanzania.

Akifafanua zaidi, kocha huyo ambaye ni raia wa Uholanzi alisema: “Nashukuru tunaendelea vizuri na michuano ya Mapinduzi ushindani upo lakini siyo ambao unaweza kutufanya tukashindwa kutimiza malengo yetu kwa sababu kwa ubora iliyokuwa nayo Singida United hivi sasa hakuna timu ambayo inaufikia,” alifunguka Pluijm.

Kocha huyo amesema kuwa ameshakutana na Yanga mara mbili, moja akipoteza na nyingine sare lakini kwa sasa kikosi chake kimekuwa bora tofauti na ilivyokuwa mwanzoni, hivyo anaamini wakikutana safari hii upepo utabadilika na Yanga wataona ubora wake.

Pia , pluijm aliweza kufunguka kuhusu mbinu anazozitumia zinazokifanya kikosi chake kuendelea kufanya vizuri kwenye mashindano ya kombe la mapinduzi . Pluijm amesema kuwa kutokana na ratiba ngumu ya michuano hiyo , wachezaji wakimaliza mechi hawapigi tena mazoezi mengine bali huwapa muda wa kupumzika na kufanyiwa masaji .

“Tunacheza mechi kila siku, hatupumziki, wachezaji wamechoka jambo ambalo kama kocha unabidi uwe makini ili mambo yaende vizuri,” alisema Pluijm.” alikaririwa akisema kocha huyo .

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com