Je, Unamfahamu kocha mpya wa Simba ?


Baada ya kuhangaika huko na kule ikisaka Kocha wa kuifundisha kwa msimu wa 2015/2016 , hatimaye wekundu wa msimbazi wamelamba dume na kufanikisha kutia sahihi kwa kocha wao mpya , Dylan Kerr (miaka 48), ambaye amesaini mkataba wa mwaka mmoja wa kuinoa timu hiyo ambapo endapo atafanya vizuri kuna kipengele kinachomruhusu kuongezewa mkataba. Dylan anategemewa kuanza kuinoa Simba kuanzia Julai Mosi ambapo ujio wake unatokea nchini Vietnam ambapo alikua akifundisha timu ya ligi kuu iitwayo , Hai Phong aliyojiunga nayo Januari mwaka 2014.

DYLAN-KERR-kocha-mpya-simba

Ukiachana na kuwa kocha mpya wa Simba, Dylan pia aliwahi kuichezea uingereza miaka ya nyuma. Historia yake ya mpira ilianzia Sheffield Wednesday mwaka 1984. Kutoka Sheffield Wednesday alichezea vilabu mbalimbali kama Arcadia Shepherds ya Afrika Kusini mwaka 1988 na  Leeds United ya uingereza mwaka 1989.Simba iliachana na Goran Kopunovic baada ya kutoafikiana katika suala la maslahi ya mkataba mpya, hivyo  Ujio wa kocha huyu unasemekana utabadilisha benchi la ufundi lote la simba ikiwa ni moja ya sharti alilotoa kocha huo ili aweze kuleta mabadiliko chanya kwenye kikosi hicho cha wekundu wa msimbazi.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com