Jerry Muro aipigia magoti TFF…


Baada ya Afisa habari wa klabu ya Yanga Bw. Jerry Muro  kutumikia kifungo chake cha mwaka mzima kwa miezi   6  hadi sasa , leo ameamua kuwa mpole na  kuandika barua ya kuomba kupunguziwa adhabu ya kufungiwa kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa mwaka mmoja.

Kamati ya nidhamu ya TFF ilimtia hatiani Jerry Muro kwa kosa la kupinga uamuzi wa TFF na kulishambulia kupitia vyombo vya habari shirikisho hilo la soka nchini ambapo kamati hiyo ilitoa adhabu ya kumfungia Muro kutojihusisha na masuala ya soka kwa mwaka mmoja pamoja na faini ya shilingi milioni tatu za Tanzania.

 

 

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , [email protected]