Klabu ya Uturuki kumtathmini Mbwana Samatta leo..


Wakati klabu ya KRC Genk anayochezea mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania , Mbwana Samatta ikiwa  na kibarua kizito leo wakati itakapomenyana na klabu ya Celta Vigo ya Hispania katika mchezo wa robo fainali ya kuwania Europa Cup , taarifa kutoka mtandao mmoja nchini Uturuki zinaripoti kuwepo kwa waangalizi kutoka klabu ya fenerbahce ya Uturuki huku wakiwa na jukumu  la kumtazama Mbwana Samatta akifanya yake uwanjani .

Ukiachana na  Samatta , waangalizi hawa pia watakua wakimuangalia Theo Bongonda ambaye ni kiungo mbelgiji anayeichezea Celta Vigo . Wakimaliza kutazama mechi ya leo waangalizi hawa wanategemewa kuelekea Uholanzi kutafuta wachezaji wengine wa kuwasajili kwenye Msimu ujao .

Kwasasa Mbwana Samatta anamkataba na KRC Genk hadi mwaka 2020 huku akiwa tayari amewafungia magoli  19 ., akitoa assist 5 katika mechi 49 alizoichezea.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com