Kocha Yanga agoma kuzungumzia kipigo cha Azam FC…


Kocha  wa Yanga, Mzambia George Lwandamina jana alikataa kabisa kuuzungumzia mchezo wa juzi dhidi ya Azam FC.

Yanga ilifungwa 4-0 na Azam juzi katika mchezo wa mwisho wa Kundi B wa Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kipigo hicho kimewashtua wapenzi na wanachama wa Yanga na bahati mbaya kesho watamenyana na mahasimu wao, Simba katika nusu fainali.

Alipoulizwa juu ya mchezo wa juzi, Lwandamina alisema; “Sina cha kusema”. Na alipoulizwa kuhusu mchezo ujao, Lwandamina akajibu pia; “Sina cha kusema”.

Matokeo hayo yanazifanya timu zote zimalize na pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja, lakini Azam FC wanakuwa juu ya Yanga kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa.

Sasa Azam itacheza na mshindi wa pili wa Kundi B katika nusu fainali, wakati Yanga Jumanne ikicheza na mshindi wa kwanza wa kundi hilo, Simba.

Mabao ya Azam juzi yalifungwa na John Bocco dakika ya pili, Yahya Mohammed (54′), Joseph Mahundi (80′) na Enock Atta Agyei (85′).

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , [email protected]