Kuelekea Simba VS Yanga kesho , yote unayopaswa kujua…


Siku ya kesho , jiji la Dar-es-salaam litakua na agenda moja tu, kwenda uwanja wa taifa kushuhudia mchezo wa Dar-es-salaam Derby kati ya Simba na Yanga , mchezo  utaotarajiwa kuanza  majira ya saa 10 Jioni .

Kama haujanunua Tiketi bado , basi bei ni kama ifuatavyo , VIP A ni shilingi 30,000/=  , VIP B na C itakua  20,000 /= na mzunguko ambao ni majukwaa ya rangi ya chungwa , kijani na bluu itakua shlingi 70,000 /=

Kuhusu Mwamuzi wa pambano la kesho ,  Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Chama, aliweka wazi kuwa Emanuel Mwandembwa kutoka Arusha ndiye atakayepuliza kipenga katika pambano hilo huku tayari kukiwa na hofu kuhusu uzoefu wake katika mapambano makubwa .

Kuhusu Mgeni rasmi katika pambano la kesho , Mkuu wa mkoa wa Dar-es-Salaam , Paul Makonda ndio atakua  mgeni rasmi ambapo atawaongoza maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu watakaojitokeza kweye Uwanja wa Taifa kushuhudia mpambano huu.

Simba na Yanga wanaingia uwanjani huku wote wakiwa na   kumbukumbu ya kutoka sare ya bao 1-1 na wapinzani wao katika mzunguko ulioisha, ambapo Simba ilitoshana nguvu dhidi ya Lipuli na Yanga ikashikwa na Mbeya City.

Simba wanaingia uwanjani  katika mchezo wa kesho wakiwa wanaongoza ligi baada ya kujikusanyia pointi 59 ikicheza michezo 25 wakati Yanga wana pointi 48 wakiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 23.

 

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com