Mambo 10 ya kujua kuhusu michuano ya kombe la Kagame kabla haijaanza kutimua vumbi…


Tunahesabu si zaidi ya wiki sasa kabla ya kuanza kwa michuano ya CECAFA Kagame Cup jijini  Dar es Salaam, Tanzania, ambapo haya ni mashindano yanayofanyika kila mwaka yakishirikisha timu za ukanda wa Afrika mashariki na kati. Kwa mwaka huu mashindano hayo yataanza kutimua vumbi siku ya jumamosi , Tarehe 18 mwezi huu na kufungwa jumapili , tarehe 2 August huku kukitegemewa bingwa mpya baada ya mabigwa watetezi El Merriekh ya Sudan kujitoa ili waelekeze nguvu kwenye ligi ya mabingwa Africa. Tukiwa tunayakaribia mashindano haya ya Kagame , hivi ni vitu 12 muhimu uvijue kuhusu michuano hii  :-

El-Merreikh-washindi-wa-cecafa-2014

1. Abaluhya FC (sasa ikiitwa AFC Leopards) ya  Kenya ilikua ni timu ya kwanza kushinda kombe hili  la CECAFA mwaka 1967  ambapo waliipa kichapo cha mabao 5 bila majibu timu ya Sunderland FC  (kwasasa Simba ) ya Tanzania japokua hawakutambuliwa  kama mabigwa.  Kutoka mwaka huo mashindano haya yalisimamishwa hadi mwaka 1974 ambapo timu ya Simba ilichukua kombe baada ya kuifunga Abaluhya FC kwenye fainali na kuwafanya Simba wawe mabingwa wa kwanza  wanaotambulika (official Winners )  wa kombe hili la Kagame .

2. Simba ya Tanzania ndio wanaoongoza kuchukua kombe hili mara nyingi  ( Mwaka 1974, 1991, 1992, 1995, 1996 na 2002) na pia wanaongoza kucheza mechi za fainali nyingi ambazo ni 11 na kama wewe unajua hisabati basi utajua kwamba ilipoteza mechi 5 za fainali sawa na APR ya Rwanda.

3. Vilabu kutoka Kenya ndio vinaongoza kuchukua kombe hili (mara 15 ) , vikifuatiwa na vilabu vya Tanzania ( Mara 11) na Uganda (Mara 5). Nchi nyingine ni kama ifuatavyo , Rwanda (mara 4) , Sudan (Mara 3) na Burundi (Mara 1) . Ukiachana na haya chakushangaza ni kwamba Kenya , Uganda na Rwanda ndio inaongoza kwa vilabu vingi kuchukua kombe hili (vitatu).

4. Mashindano haya yalikua yakijulikana kama  mashindano ya vilabu ya CECAFA mpaka mwaka 2002 ambapo yalibadilishwa jina na kua Kagame CECAFA Cup , yote haya yalikuja baada ya udhamini wa rais wa Rwanda Paul Kagame wa dola  30,000 kwa mshindi wa kwanza ,  20,000 kwa mshindi wa pili na  $ 10,000 ka mshindi wa tatu.

5. Kocha wa sasa wa Sofaaka ya Kenya , Sam Timbe ndio anarekodi ya kuchukua kombe la Kagame mara nyingi zaidi ambapo alichukua akiwa na vilabu vya SC Villa (2004), Police FC (2005), Atraco (2009) na  Yanga(2011).

6. Ni fainali sita tu zimewahi kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti ukianza na mwaka 1978 ambapo  KCC FC iliifunga Simba 3-2  baada ya droo ya bila magoli,  mwaka  1986   El Merriekh iliifunga Yanga 4-2 kwa mikwaju ya penalti baada ya droo ya   2-2 . Nyingine ni mwaka  1992 (Simba iliifunga Yanga 5-2 baada ya droo ya  a 1-1 ), mwaka 1995  Express FC ilifungwa na  Simba 5-3 kwa matuta baada ya droo ya  1-1 , mwaka 1999 Yanga waliifunga  SC Villa 4-1 baada ya droo ya  1-1 na mwisho mwaka  2001 ,  Tusker iliifunga Oserian  3-0 katika fainali iliyozishirikisha timu zote za Kenya baada ya droo ya bila kufungana.

7. Mara 8 , timu kutoka nchi moja zimekutana kwenye fainali huku  mara zote timu hizo zikitokea  Tanzania na Kenya tu. Fainali hizo ni  Simba – Yanga (1975), Gor Mahia – Abaluhya (1980), Gor Mahia – AFC Leopards (1985), Yanga – Simba (1992), AFC Leopards – Kenya Breweries (1997), Tusker – Oserian (2001), Yanga – Simba (2011) and Yanga – Azam (2012).

8.  Tanzania  imekua mwenyeji wa mashindano haya mara 11 huku mashindano yanayotegemewa kuanza wiki ijayo yakifikisha idadi ya 12 . Kenya  inafuatia ikiwa ni mara tisa (9) na Uganda mara sita (6).

9.  Mashindano haya hayakufanyika mara mbili tu tokea yaanzishwe na kutambulika  mwaka 1974. miaka hiyo ilikua 1990 na 2010.

10. Mara zote  11 Tanzania ilivyowahi kua  mwenyeji wa mashindano haya  , Vilabu vya Tanzania vilishinda mashindano haya ukijikumbusha mwaka 2011 na 2012 .

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com