Matatu usiyoyajua kuhusu Simon Msuva


Simon Happygod Msuva wiki hii alifanikiwa kufanya interview na mtandao wa MillardAyo ambapo alifunguka kuhusu mambo kadhaa yakiwemo haya ambayo tunadhani ungependa kuyafahamu kuhusiana na maisha yake nje ya soka.

1- Baba na mama yake mwanzoni walikuwa hawamsapoti kucheza soka walitaka ajikite katika masomo zaidi “Nilianza kucheza soka toka nasoma shule ya msingi wazazi walikuwa hawataki nicheze soka walitaka nisome tu ila baada ya kumaliza form 4 waliamua kuniunga mkono”  alisema Msuva

Simon-Msuva-Bongosoka-Yanga-MillardAyo

2- Fedha yake ya kwanza kubwa kushika ni laki tatu ambayo alisajiliwa na klabu ya Moro United wakati huo na kuamua kuitoa sadaka ” Nilisajiliwa na Moro United kwa laki tatu lakini baada ya kushauriana na baba na mama tukaamua kuitoa sadaka yote ili mungu anifungulie milango” 

Simon-Msuva-Yanga-bongosoka

3- Kutokana na umahiri wake uwanjani aliwahi kupewa zawadi ya gari na mashabiki wa Yanga ” Sikutarajia kuwa mashabiki watanipa zawadi ya gari ila nilihisi kwani washawahi kuniuliza napenda gari gani kati ya Nissan X-Trail, Passo, Opah na Altezza nikachagua Altezza, siku wakanipigia simu kwenda nikakabidhiwa funguo za gari” 

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com