Matokeo Mapinduzi Cup: SImba yaibamiza URA goli 1 , kuwavaa Mtibwa nusu fainali


Mabingwa wa tetezi wa kombe la mapinduzi Simba SC wamefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali na kuiepuka Yanga SC katika hatua ya nusu fainali baada ya leo kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya JKU ambayo leo imeiga rasmi michuano hiyo.

Katika mchezo huo wa mwisho wa kundi A uliochezwa katika uwanja wa Amani visiwani Zanzibar Simba SC walipata goli lao pekee katika dakika ya 65 kupitia kwa Jonas Mkude akimalizia krosi ya Emery Nimubona.

Simba SC waliuwanza mchezo wakiwa wanatumia mfumo wa 3-5-2 ambao ulishindwa kuzaa matunda na kupelekea kushambuliana kwa zamu na JKU katika kipindi chote cha kwanza.

Simba-Mapinduzi-cup

Katika dakika ya 45 amanusura JKU waandike goli pale mshambuliaji wa JKU aliposhindwa kmalzia mpira uliotemwa na Manyika kufuatia mpira wa adhabu na kupelekea mchezo kwenda mapumziko wakiwa bado hawajafungana.

Kipindi cha pili Simba SC waliwapumzisha Kiongera, Hamisi Kiiza na Awadhi Juma na nafasi zao kuchukuliwa na Danny Lyanga, Ibrahim Ajibu na Mwinyi Kazimoto.

Mabadiliko hayop yalioongeza kasi ya Simba SC na katika dakika ya 60 walilisakama lango la JKU kwa dakika 5 na kufanikiwa kuandika goli kupitia kwa Mkude.

Kuingia kwa goli hilo kulipunguza kasi ya Simba SC na kuifanya JKU kurejea mchezoni na kuanza kupeleka mashambulizi ambapo walifanikiwa kutengeneza nafasi 3 ambazo walishindwa kuzitumia.

Hadi mpira unamalizika Simba SC waliocheza soka safi katika kipindi cha pili goli 1-0 JKU hawajpata kitu.

Matokeo ya mchezo huo unapelekea Simba SC kukutana na Mtibwa Sugar mchezo utakao chezwa usiku katika uwnaja wa Amani siku ya jumapili, huku kukitanguiliwa na mchezo kati ya Yanga na URA saa kumi alasiri.
MICHEZO YA NUSU FAINALI
YANGA SC Vs URA (saa 10:15 alasiri)
SIM BA SC Vs MTIBWA SUGAR (saa 2:15 usiku)

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com