Mohamed Salah kucheza kombe la dunia


Mshambuliaji mahiri raia wa misri , Mohamed Salah anategemewa kurudi uwanjani ndani ya wiki 3 tayari kuisaidia timu yake ya taifa ya Misri kwenye mashindano ya kombe la dunia yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 14 , April nchini misri .

Salah  alilazimika kutolewa nje ya uwanja baada ya kupata majeraha ya bega katika mchezo wa fainali ya klabu bingwa ulaya ambapo klabu yake ya Liverpool ilifungwa goli  3-1 na Real Madrid juma lililopita .

Salah aliwasili jijini  Valencia siku ya jumanne kwa matibabu ya bega lake lililoumia na tayari madaktari wa timu ya taifa ya misri wameshaanza kumuhudumia .

Chama cha soka nchini Misri kupitia akaunti yake ya Twitter kilithibitisha kua Salah anategemewa kurudi uwanjani wiki 3 zijazo .

Uwezekano mkubwa wa salah kuanza kuichezea Misri ni katika mechi ya mzunguko wa pili dhidi ya wenyeji Urusi unaotegemewa kupigwa katika dimba la Saint Petersburg tarehe 19 mwezi wa 6 .

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com