Mzimbabwe Singida United Usipime


Mshambualiaji wa Kimataifa wa Zimbabwe , Mitchele Katsvairo , ameonyesha kua tishio katika klabu yake mpya ya Singida United ,  baada ya kufunga magoli mawili katika mechi 3 za ligi kuu ya Vodacom.

Kocha mkuu wa Singida United , Hans Van Pluijm tayari ameonyesha imani kubwa na nyota huyu wa kigeni huku akimsifia kua ni straika mzuri .

“Nafahamu Ubora wake unategemea pia na uchezaji wa wengine , lakini nina kikosi kipana kinachoweza kufanya vizuri zaidi msimu huu . Naamini itakua hivyo. ” alikaririwa akisema .

Katsvairo ni moja ya usajili uliofanywa na Singida United katika lala salama za dirisha la usajili ambapo alisajiliwa kutokea klabu ya Kaizer Chief Ya nchini Afrika Kusini kwa mkopo baada ya makubaliano baina ya Vilabu hivyo.

 

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com