Ratiba ya ligi kuu Tanzania bara msimu wa 2017-2018 yatoka…


Msimu mpya wa ligi kuu ya vodacom Tanzania bara unatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 26 , Agosti huku michezo saba ikitegemewa kuchezwa siku ya Ufunguzi .

Ukiachana na Mechi za ufunguzi , mchezo wa ngao ya jamii kati ya watani wa jadi , Simba na Yanga unategemewa kupigwa katikati ya wiki , siku ya jumatano , tarehe 23 Agosti kupisha ratiba ya mechi ya raundi ya pili ya michuano ya CHAN kama Taifa Stars ikifanikiwa kuifunga Rwanda kwenye mechezo wa raundi ya kwanza .

Jumamosi , Tarehe 26 , Agosti , 2017

Ndanda FC VS Azam FC

Mwadui FC  VS Singida

Mtibwa Sugar VS Stand United

Simba SC VS Ruvu Shooting

Kagera Sugar VS Mbao FC

Njombe Mji VS Prisons

Mbeya City VS Majimaji

 

Jumapili , Tarehe 27 , Agosti , 2017

Yanga SC VS Lipuli FC

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com