Robo fainali Kagame Cup Kuanza kutimua vumbi leo…


Hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup 2015) inatarajiwa kuanza leo  Jumanne kwa michezo miwili kuchezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Mchezo wa kwanza utakua ni kati ya Mabingwa mara tatu wa michuano hiyo timu ya APR ya Rwanda itakayotoshuka dimbani saa 7:45 mchana kucheza na vijana wa Kwesi Appiah timu ya Al Khartoum kutoka nchini Sudan. Saa 10:15  jioni, Gor Mahia mabingwa mara tano wa michuano ya Kagame watashuka dimbani kucheza na Malakia kutoka Sudan Kusini, viingilio vya michezo hiyo ya jumanne cha chini kitakua ni elfu tatu (3,000) na kiingilio cha juu kitakua ni elfu kumi na tano (15,000).
Robo-Fainali-CECAFA-Kagame-Cup-bongosoka-Yanga-Azam-APR-Gor-Mahia
Robo fainali zitaendela siku ya jumatano, ambapo michezo miwili itachezwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam huku macho na masikio ya wapenzi wa mpira Afrika Mashariki yakielekezwa kwa mchezo kati ya Azam FC dhidi ya Yanga SC. Kabla ya mechi hiyo ya wapinzani wa soka nchini Tanzania kuchezwa majira ya saa 10 jioni, mchezo wa kwanza utazikutanisha timu za KCCA ya Uganda dhidi ya Al Shandy kutoka nchini Sudan. Viingilio vya mchezo wa siku ya jumatano, kiingilio cha chini ni shilingi elfu tano (5,000) na kiingilo cha juu kitanua ni elfu ishirini (20,000). Katika hatua hiyo ya robo fainali endapo timu zitacheza kwa dakika 90 na mchezo kumalizika kwa sare, hatua itakayofuata ni kumpata mshindi kwa matuta (penati).
CECAFA YAIPA ONYO GOR MAHIA
Vilevile baraza la Vyama vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiandika barua ya onyo klabu ya Gor Mahia kutoka nchini Kenya kufuatia kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu katika michezo yake miwili ya kwanza. Katika barua hiyo ya CECAFA kwenda kwa Gor Mahia, imeutaka uongozi huo kuhakikisha kocha wake Frank Nutal na kikosi kizima kinafuata taratibu za mashindano na kanunu zilizopo zinazoongoza michuano hiyo.Kamati ya uendeshaji wa michuano hiyo (LOC) iliwasilisha malaliko kwa uongozi wa CECAFA juu ya tabia ya utovu wa nidhamu iliyoonyeshwa na kocha mkuu wa Gor Mahia, na kitendco cha kuvunja kitasa cha mlango ili kuingia uwanjani.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com