Samatta , Rooney watupia , Genk ikitoka sare na Everton…


Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta leo ameweza kuisaidia timu yake ya KRC Genk kutoka Sare ya bao 1 – 1 dhid ya Everton ya nchini Uingereza , mchezo ulioudhuriwa na   maelfu ya mashabiki nchini Ubelgiji .

Everton ndiyo ilikuwa ya kwanza kupata goli kupitia kwa Wayne Rooney dakika ya 35 katika kipindi cha kwanza, ambapo Samatta alifanikiwa kuisawazisha dakika ya 55 ya kipindi cha pili na hivyo mchezo kumalizika kwa Genk 1-1 Everton.

Huu ni mwanzo mzuri kwa Mbwana  Samatta kuelekea  kuanza kwa  msimu wa 2017/18 wa ligi nchini Ubelgiji huku ikikumbukwa kua   ndoto ya Samatta  katika soka ni pamoja na kucheza  ligi kuu ya Uingereza maarufu kama EPL .

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com