Simba bingwa ngao ya jamii , yaifunga Yanga kwa matuta….


Klabu ya wekundu wa msimbazi , Simba imenyakua Ngao ya jamii baada ya  kuifunga Yanga SC kwa penati 5-4. Katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua huku kukiwa na upinzani mkubwa baina ya mahasimu hao wa jadi,  Hadi dakika 90 zinamalizika hakuna timu iliokua imeona lango la mwenzake na kusababisha mshindi kuamuliwa kwa mikwaju ya penalti .

Yanga ilianza penalti hizo vibaya kwa Kelvin Yondani na baadaye Juma Mahadhi kukosa huku walipopata ni nahodha Thaban Kamusoko, Pappy Tshishimbi, Ibrahimu Ajib, Donald Ngoma.

Wafungaji wa Simba katika penalti hizo ni nahodha Method Mwanjali, Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima, Shiza Kichuya wakati Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akikosa kabla ya Mo Ibrahimu kufunga penalti ya sita iliyoipa Simba ubingwa .

 

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com