Simba kuwakosa Mavugo , Niyonzima…


Washindi wa pili kwenye kombe la mapinduzi mwaka jana , Kkabu ya wekundu wa msimbazi , SImba inategemea kuanza mbio za kuwania kombe la mapinduzi jioni ya leo pale watakapochuana na Mwenge Saa 10:30 jioni .

Simba inaingia kwenye michuano hii ya mapinduzi bila nyota wake Laudit Mavugo ambaye yupo kwao Burundi na Haruna Niyonzima ambaye bado anauguza maumivu ya kifundo cha mguu .

Simba imeenda kwenye michuano  ya Mapinduzi na wachezaji 24 wakiwemo Emmanuel Okwi na Shomary Kapombe waliokua majeruhi .

Simba ipo Kundi A pamoja na, Azam, URA ya Uganda, Jamhuri na Mwenge .

Baada ya mchezo wa leo , Simba wanategemewa kucheza tena Januari 4  ambapo watakutana  na Jamhuri Saa 2:15 usiku, kabla ya kumenyana na Azam FC Januari 6 na kuhitimisha mechi zake za Kundi A kwa kumenyana na URA Januari 8, 2018 Saa 10:30 jioni.

Mechi za makundi zinatarajiwa kukamilishwa Januari 8, wakati Januari 9 itakuwa mapumziko na Nusu Fainali zitafuatia Januari 10, kabla ya kilele mashindano kwa mchezo mtamu wa fainali Januari 13, ambao utahudhuriwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi visiwani humo, Dk. Ali Mohammed Shein.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com