Simba VS Yanga kuchuana nusu fainali mapinduzi cup kesho…


Klabu za Simba na Yanga zitakutana katika mchezo wa nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi utakaofanyika  Kesho ,  Jumanne kwenye Uwanja wa Amaan , Zanzibar .

Timu hizo zitakutana mwaka huu kwa mara ya kwanza baada ya jana Simba kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Jang’ombe Boys na katika Kundi A.

Yanga wenyewe wanakutana na Simba baada ya kumaliza wa pili katika Kundi B kufuatia kipigo cha `mbwa mwizi’ cha mabao 4-0 kutoka kwa Azam FC katika Kundi A.

 

Katika mchezo huo wa jana, Laudit Mavugo aliing’arisha Simba kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuifungia mabao mawili. Simba ilicheza vema kipindi chote cha kwanza huku washambuliaji wake Mavugo na Shiza Kichuya wakionekana kung’ara zaidi kwenye safu hiyo.

Iwapo Mavugo angetuliza akili katika kupiga mashuti langoni mwa Jang’ombe, angeipatia mabao mengi timu yake hiyo kwenye kipindi cha kwanza. Simba ilipata bao la pili lililoiwezesha kufikisha pointi 10 baada ya Mavugo kufunga tena.

Mchezaji huyo aliuchukua mpira kwa kisigino na kisha kuwatoka mabeki wa Jang’ombe na kisha kuachia shuti kali lililomwacha kipa wa Jang’ombe, Hassan Haroun chini. Simba iliendelea kufanya mabadiliko ambapo ilimtoa Mavugo na kisha kumuingiza na kumuingiza Jamal Mnyate.

Dakika ya 63 Simba inamtoa mchezaji wake Juma Lauzio na kisha anaingia Moes Kitandu. Jang’ombe ilifanya mabadiliko kwa kumtoa Juma Ali Juma na kumwingiza Amur Suleiman hapo ikiwa ni dakika ya 67.

Jang’ombe ilijitaidi kufanya mashambulizi ya mara kwa mara bila ya mafanikio ambapo dakika ya 70 ilifanya shambulizi kupitia mchezaji wake Khamis Mussa ambapo mchezaji huyo aliachia shuti lililopiga nje.

Simba dakika ya 72 ilimtoa mchezaji wake Shiza Kichuya na kumuingiza Haji Ugando huku Jang’ombe ikimuingiza Abubakar Mkubwa na kumtoa Ibrahim Novat.

Mavugo alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo.

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , [email protected]