Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba , Jana illiweza kuwaacha mahasimu wenzao , Yanga kwa pointi 3 katika msimamo wa ligi kuu Tanzania bara baada ya kuitundika klabu ya Njombe Mji mabao 2- 0 katika mechi ya kiporo iliyopigwa kwenye uwanja wa Sabasaba mkoani Njombe .
Magoli yote ya Simba yalifungwa na mshambuliaji wao hatari , John Bocco ambapo dakika ya 17 aliachia shuti kali lililotinga moja kwamoja wavuni na kmuacha kipa wa Njombe mji bila la kufanya .
Bocco aliongeza goli la pili kipindi cha pili cha mchezo katika dakika ya 64 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Shomari Kapombe na kuuweka mpira moja kwa moja wavuni .
Kwa ushindi walioupata Simba , wanaendelea kuongoza ligi wakiwa na pointi 49 nyuma ya Yanga yenye pointi 46 huku timu zote zikiwa na michezo sawa kwasasa .
Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , [email protected]
Soma Habari zaidi kuhusu: ligi kuu tanzania bara Njombe Mji Simba