Simba yasonga mbele kombe la shirikisho , kukutana na timu hii…..


Klabu ya wekundi wa Msimbazi , Simba imefanikiwa kusonga mbele kwenye michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuitungua ugenini klabu ya Gendamarie  ya Djibouti bao 1 – 0 , bao lililoweka wavuni na mshambuliaji wao hatari , Emmanuel Okwi katika dakika ya 53 ya mchezo .

Kwa ushindi huu walioupata , Simba inafuzu kwa jumla ya mabao 5 – 0 , baada ya kuondoka na ushindi wa goli 4 – 0 katika mchezo wa kwanza wa michuano hii .

Simba watakutana na klabu ya Al Masry  ya Misri katika hatua nyingine ya michuano hii ambapo mafarao hao nao wamefanikiwa kusonga mbele kwa jumla ya mabao 5 – 2 baada ya kufungwa mabao 2-1 wakiwa ugenini dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia na kuibuka na ushindi wa mabao 4 – 0 wakiwa nyumbani .

Mechi ya kwanza itaanzia jijini Dar es Salaam, kabla ya Simba kufunga safari na kwenda Misri kumalizia ngwe hiyo inayotarajia kuwa ngumu.

Simba ina heshima kubwa kwa kuwa imewahi kuivua ubingwa na kuing’oa mashindano Zamalek ya Misri, timu kubwa ya pili na moja ya klabu maarufu barani Afrika.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com