Taifa Stars yaaga CHAN , yatoka sare na Rwanda…


Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetolewa katika michuano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN) baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Rwanda ‘Amavubi’ katika mchezo wa marudiano .

Katika mchezo wa awali uliofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza timu hizo zilitoka sare ya bao moja hivyo Stars kutolewa kwa faida ya bao la ugenini.

Katika mchezo huo Stars ilicheza vizuri tofauti na ule wa kwanza kwa kutengeneza nafasi nyingi kutokana na mabadiliko makubwa ya kiufundi lakini washambuliaji walioongozwa na John Bocco ‘Adebayor’ walishindwa kupata bao kutokana na umakini mkubwa wa walinzi wa Amavubi.

Stars iliingia katika michuano hiyo ikiwa na kumbukumbu nzuri ya kumaliza nafasi ya tatu ya michuano ya COSAFA iliyofanyika Afrika Kusini mapema mwezi huu lakini matokeo ya leo ya sare yameifanya kutolewa nje mashindano.

Amavubi itakutana timu ya Uganda ‘The Cranes’ katika hatua ya mwisho ya michuano hiyo baada ya kuiondoa Sudan Kusini.

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com