Thomas Ulimwengu apata ofa ulaya…


Hatimaye mshambuliaji wa timu ya taifa ya Tanzania , Thomas Ulimwengu ameanza kupata ofa kutoka klabu mbalimbali barani Ulaya huku meneja wake , Jamal Kisongo akigoma kutaja timu hizo huku akidokeza kua ofa moja imetoka klabu inayoshiriki ligi kuu ya Uholanzi .

Kisongo aliendelea kusema kua Klabu hiyo ya nchini   Uholanzi inatarajia kuleta ofa ya  kumuhitaji Ulimwengu hapo kesho .

Kisongo amesema kuna matarajio ya Ulimwengu kupata timu Ulaya na amewataka Watanzania wawe wavumilivu na kumuombea kijana huyo, ili afanikiwe kucheza Ulaya.

Ulimwengu, na Mbwana Samatta anayecheza Ubelgiji kwa sasa kwenye klabu ya Genk, tangu mwezi wa Januari mwaka uliopita, wote walikuwa wakiichezea TP Mazembe ya DR Congo kabla ya kumaliza mikataba yao mwaka uliopita.

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , [email protected]