Ukweli kuhusu Mohamed Dewji kuinunua Simba huu hapa..


Kumekua na taarifa mbalimbali zisizo rasmi zinazomuhusisha Mohamed Dewji “MO”  ,  bilionea anayeshika namba 24 Afrika  kuhusu kuinunua klabu ya Simba ambapo yeye mwenyewe aliwahi kukiri wazi kupitia kipindi cha Mkasi TV kuhusu uwezekano wa ununuzi huo .

Kuhusu Swala hilo la ununuzi huo , sasa viongozi wa Simba wameamua kufunguka kuhusu taarifa hizo ambapo msemaji wa Simba Haji Manara  amekiri kua  bado klabu haijapokea barua rasmi kutoka kwa MO .

Mohamed-Dewji-kuinunua-Simba-bongosoka

“Ukweli ni kuwa hakuna mfanyabiashara yoyote au tajiri yeyote aliyetuma barua rasmi ya kuomba kuinunua Simba, haya maneno yanazungumzwa tu, kama klabu hatujapata barua. Ni kweli binafsi nimeiona interview ya MO ila interview ya MO haitoshi kusema ndio taarifa yake rasmi, ukweli bado klabu haijapokea barua yoyote ya mtu kuomba kuinunua Simba”

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com