Wachezaji 9 ambao Tayari wamesajiliwa na Simba…


Klabu ya wekundu wa Msimbazi , Simba tayari imekamilisha usajili wa wachezaji 9 kwa ajili ya msimu mpya wa ligi kuu 2017/2018  na kombe la shirikisho Afrika baada ya kutoshiriki kwa takribani misimu minne sasa.

Simba tayari imeshatumia zaidi ya shilingi milioni 400  katika usajili wa msimu huu . Wafuatao ni wachezaji ambao tayari wameshakamilisha usajili Simba :-

Emmanuel Okwi (SC Villa)
Emanuel Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili (2) kujiunga na Simba akitokea Sc Villa ya Uganda, winga huyo atakuwa ni mmoja wa nyota wapya  kuanzia msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na mashindano mengine ikiwa ni pamoja na michuano ya Afrika (Caf Confederatio Cup).

John Bocco (Azam)
Kama ilivyo kwa mlinda mlango, Aishi Manula, Bocco naye amejiunga na Simba akitokea Azam kwa dau linalokadiliwa ni milioni 35, kutokana na ubutu wa washambuliaji wa Simba msimu uliopita ndiyo sababu ya benchi la ufundi kuamua kumuongeza Bocco kwenye idara hiyo .

Aishi Manula (Azam)
zaidi ya milioni hamsini zimetumika kuipata saini ya mlinda mlango huyo wa timu ya taifa Tanzania , Aishi Manula amejiunga na Simba akitokea klabu ya Azam aliyodumu nayo kwa zaidi ya miaka 6 na kufanikiwa kushinda mataji mbali mbali na klabu hiyo.

Shomary Kapombe (Azam)
Kapombe amesaini mkataba wa miaka miwili ndani ya Simba, Mchezaji huyo mahiri amerudi nyumbani akitokea Azam FC aliyojiunga nayo baada ya kuacha soka la Ufaransa miaka minne nyuma .

Jamal Mwambeleko (Mbao FC)
Mlinzi wa kushoto kutoka klabu ya Mbao Fc ya Mwanza amesajiliwa kwa dau linalokadiliwa milioni 25 za kitanzania, Mwalmbeleko amekuja kwa ajili ya kumpa changamoto Mohammed Hussein ambaye ameonekana hana mbadala kwenye nafasi anayo cheza

Yusuph Mlipili (Toto Africans)
Ametokea klabu ya Toto Africans aliyoitumikia msimu uliopita, Mlipili ni beki wa kati mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi zote za ulinzi, anakuja kurithi mikoba ya ya Method  Mwanjale ambaye ana nafasi kubwa ya kuachwa kwa ajili ya msimu ujao

Ally Shomary (Mtibwa Sugar)
Baada ya Simba kuachana na walinzi wa kulia, Javier Bukungu na Hamad Juma kwa ajili ya msimu ujao, nafasi hiyo itazibwa na Ally Shomary nyota kutoka klabu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro, ambaye ana uwezo mkubwa wa kuimudu nafasi hiyo

Emmanuel Mseja (Mbao FC)
Mseja aliyesaini mkataba wa miaka miwili Simba SC akitokea klabu ya Mbao aliyoichezea msimu uliopita , mlinda mlango huyo  alikuwa kipa wa akiba wakati wote msimu uliopita katika kikosi cha Mbao FC, baada ya Erick Ngwengwe na Benedict Haule waliodaka kwa awamu.

Salum Mbonde (Mtibwa Sugar)
Beki wa kati kutokea Mtibwa Sugar, Salum Mbonde asaini mkataba wa miaka 2 kuichezea klabu ya Simba, Mbonde anatua Simba baada ya kuwa na taarifa kuwa beki Abdi Banda amejiunga na timu ya Baroka ya Afrika Kusini.

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com