Watakaoanza leo Taifa Stars VS Rwanda…


TIMU ya soka ya Taifa (Taifa Stars) itavaana  na Rwanda (Amavubi) katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kushiriki fainali zijazo za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) mwaka 2018 yatakayofanyika nchini Kenya .

Mchezo wa leo unategemewa kupigwa katika uwanja wa Kigali majira ya saa 9:30  huku katika mchezo wa kwanza timu hizi zikitoka sare ya 1 – 1 , mchezo uliopigwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza .

Ili Taifa Stars isonge mbele kwenye mchezo wa leo italazimika kuondoka na ushindi au sare ya 2 – 2 au zaidi .  Mshindi wa leo ataumana na mshindi kati ya Uganda na Sudani Kusini  katika hatua ya mwisho ya mchujo inayotegemewa kufanyika mwezi ujao .

Kikosi cha Taifa Stars kitakachoanza leo dhidi ya Amavubi ni kama ifuatavyo :-

1. Aishi Manula
2. Boniphace Maganga
3. Gadiel Michael
4. Erasto Nyoni
5. Salim Mbonde
6. Himid Mao
7. Simon Msuva
8. Mzamiru Yassin
9. John Bocco
10. Raphael Daudi
11. Shiza Kichuya

Kikosi cha akiba

12. Said Mohamed
13. Hassan Kessy
14. Nurdin Chona
15. Salimin Hoza
16. Said Ndemla
17. Joseph Mahundi
18. Stamili Mbonde

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com