Yanga kuwavaa washelisheli leo ligi ya mabingwa Afrika


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara , Klabu ya Yanga itashuka  Dimbani leo kumenyana  na Mabingwa wa Shelisheli , klabu ya St Louis katika uwanja wa uhuru jijini Dar-es-salaam katika mchezo wa kwanza wa michuano ya Ligi Mabingwa Afrika hatua ya mtoano ambapo mechi ya marudiano ikitarajiwa  kupigwa  tarehe 21 Februari katika visiwa vya shelisheli .

Klabu ya Yanga itaingia dimbani bila nyota wake wanne ambao ni  Donald Ngoma, Abdalah Shaibu, Yahana Nkomola na Amiss Tambwe .

Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema, mchezo wa leo ni muhimu kwa timu yake na kwani utaisaidia Yanga kufikia malengo yake katika michuano ya kimataifa.

Kwa upande wake kocha mkuu wa St Louis ya Shelisheli Michel Renald amesema wamekuja kucheza na yanga na wanaiheshimu na  watahakikisha wanautumia vyema kupata matokeo yatakayowawezesha kusonga mbele katika ligi ya Mabingwa.

Mchezo huo unatarajia kuwa mwepesi kwa upande wa Yanga kutokana na timu ya St Louis haina uzoefu wowote katika michezo ya kimataifa hasa hii michezo ya vilabu Bingwa Afrika.

Wawakilishi wengine wa Tanzania kwenye michuano hiyo, Zimamoto ya Zanzibar ambayo leo inaikaribisha Wolaitta Dicha wa Ethiopia Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com