Yanga nayo yatinga nusu fainali Mapinduzi Cup..


Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kutinga  nusu fainali ya michuano ya Kombe la Mapinduzi 2017 baada  kuwafunga timu ya Zimamoto ya visiwani Zanzibar mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa jioni ya leo katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mabao mawili ya Yanga  yalifungwa na winga wake , Simon Msuva katika kipindi cha kwanza cha mchezo . Msuva alifunga bao la kwanza dakika ya 11 akimalizia mpira wa adhabu wa Nahodha na kiungo wa kimataifa wa Rwanda, Haruna Niyonzima .


Bao la pili na la nne kwake katika mashindano hayo alifunga dakika ya 21 akiiwahi pasi ndefu ya Thabani Kamusoko na kumtoka beki Shaffi Rajab kabla ya kumchambua tena Mwinyi Abbas.

Ushindi wa leo wa Yanga  unaifanya iendelee kuongoza Kundi B kwa kufikisha jumla ya point 6 na magoli nane huku ikiwa haijaruhusu   goli hata moja langoni kwake .

Yanga wamebakiza mchezo mmoja dhidi ya Azam FC watakaocheza nao siku ya jumamosi ya  January 7  , saa 2 : 15 usiku katika uwanja wa Amaan.

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , [email protected]