Yanga safi CAF , yatinga makundi ikijinyakulia mamilioni…..


Klabu ya Yanga leo imefanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya kuitoa klabu ya Wolaita Dicha kwa jumla ya mabao 2 Р1 ikiwa ni baada ya kushinda kwenye mchezo wa nyumbani kwa mabao 2 Р0 na kufungwa bao 1 Р0 katika mchezo uliopigwa ugenini leo katika uwanja wa kimataifa wa Hawwasa nchini Ethiopia  .

Bao la pekee la mchezo wa leo lilitupia dakika ya pili ya mchezo na mchezaji raia wa Togo , Arafat Djako baada ya mpira mzuri wa kona kwenda moja kwa moja na kumpita beki ambaye alishindwa kuuokoa na Djako kuweka mpira wavuni .

Kutokana na matokeo hayo, Yanga itasonga mbele katika hatua hiyo na itaweka kibindoni kiasi cha zaidi ya  Sh. 600 mil kutoka CAF.

Safari ya Yanga katika hatua hiyo, ilianza kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika iliifunga St Luis ya Shelisheli jumla ya mabao 2-1, ikafungwa na Town Ship ya Botswana 2-1 ikadondoshwa kwenye kombe la shirikisho.

Huu ni mwaka wa tatu mfululizo, Yanga inaangukia kwenye kapu la kuwania kucheza hatua ya makundi ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kutolewa Ligi ya Mabingwa na mara ya nne kwa ujumla kihiostoria.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com