Yanga , Simba , Singida United zapeta kombe la mapinduzi…


Klabu za Yanga ,  Simba na Singida United zimeweza kuibuka na ushindi katika michezo ya mwendelezo wa kuwania kombe la Mapinduzi inayoendelea visiwani Zanzibar .

Baada ya kuitungua Mlandege ya Unguja 2 – 1 katika mchezo wake wa kwanza , klabu ya Yanga imeweza kuibuka na ushindi mwingine mzuri leo dhidi ya JKU ya Unguja baada ya kuitundika bao 1 – 0 , bao lililopatikana dakika ya 89 ya mchezo kupitia kwa beki wake , Hassan Kessy baada ya kupokea basi safi ya kisigino kutoka kwa Pius Buswita . Ushindi huu wa Yanga unaifanya ifikishe pointi 6 baada ya mechi mbili .

Kwa upande wa Simba , nayo imefanikiwa kuwatoa kimasomaso mashabiki wake hasa baada ya kutoka sare ya bao 1 – 1 na mwenge ya Pemba kwenye mchezo wake wa Kwanza . Simba leo , imeibuka na ushindi wa goli 3 – 1 dhidi ya Jamhuri ya Pemba . Mabao ya Simba yalitiwa wavuni na beki wake mpya  Asante Kwasi , John Bocco na Moses Kitandu huku lile pekee la kufutia machozi la Jamhuri likifungwa na Moses Nassoro .

Kwa matokeo hayo Simba imekaa nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi A baada ya kujikusanyia pointi nne ikiwa ni pointi mbili tu nyuma ya vinara Azam FC wenye sita.

Katika mchezo mwingine uliopigwa leo , Singida United iliendeleza ushindi kwa kuitwanga Taifa ya Jang’ombe kwa mabao 3-1.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com