Yanga , Simba zasajili wawili leo..


Katika kuhakikisha kila timu inajidhatiti katika mbio za ligi kuu Tanzania bara na Mashindano ya kimataifa , klabu  za Simba na Yanga zimekamilisha sajili mbili kila mmoja kwa siku ya leo .

Kwa upande wa Simba  , wao wamefanya usajili wa nyota wawili kwa mpigo ambao ni  kipa namba mbili wa Taifa Stars, Said Mohammed ‘Nduda’ na beki, Erasto Nyoni.

Usajili huo wa Simba umekuja katika hali isiyotarajiwa kutokana na awali timu hiyo kuonekana kama imejiimarisha vilivyo, lakini leo uongozi wa timu hiyo  umethibitisha kuwasanisha wachezaji hao kwa mikataba ya miaka miwili kila mmoja.

Nduda aliyesaini akitokea Mtibwa Sugar, amesajiliwa maalum kwa kumpa changamoto Aishi Manula ambaye pia amejiunga na timu hiyo akitokea Azam FC.

Katika michuano ya Cosafa iliyoisha hivi karibuni na Taifa Stars kushika nafasi ya tatu, Nduda aliibuka kipa bora wa michuano hiyo ingawa alidaka mchezo mmoja tu wa kuwania mshindi wa tatu.

Kwa upande wa Nyoni aliyesaini akitokea Azam, amesajiliwa mahususi kuziba pengo la Abdi Banda aliyejiunga na Baroka FC ya Afrika Kusini.

Kwa Upande wa Klabu ya Yanga nayo imemsainisha mkataba mpya wa miaka miwili kiungo Mzimbabwe, Thaban Kamusoko huku pia ikimsajili kipa wa Serengeti Boys, Ramadhani Kabwili.

Taarifa iliyotolewa na Yanga kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Hussein Nyika ni kwamba Kamusoko ameongeza mkataba huo baada ya kufikia makubaliano ya mambo kadhaa.

Katika kuimarisha lango lao, Yanga pia imefanya usajili wa Kabwili ambaye alikuwa na Serengeti Boys katika michuano ya Vijana Afrika mwaka huu nchini Gabon.

Usajili umeifanya Yanga kukamilisha usajili wa nyota wanne wapya ambapo awali ilimsainisha kipa wa African Lyon, Youthe Rostand, beki Abdallah Shaibu pamoja na mshambuliaji Ibrahim Ajib

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com