Yanga , Singida United zatinga nusu fainali mapiduzi cup , Azam FC bado bado…..


Klabu za Yanga na Singida United za Tanzania bara zimefanikiwa kutinga kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Mapinduzi cup yanayoendelea Visiwani Zanzibar huku klabu ya Azam FC ikiwa bado bado ikisubiri mechi yake ya mwishi dhidi ya Simba itakayoamua hatma yake .

Singida United ndio ilikua timu ya kwanza kutinga hatua ya Nusu Fainali  baada ya kuitungua Mlandege goli 3-0 na  kufikisha pointi tisa  kufuatia kushinda mechi tatu mfululizo katika Kundi B. Mechi ijayo Singida United  itashuka uwanjani kucheza dhidi ya JKU ikiwa ni mchezo wake  wa nne.

Kundi B lina timu sita ambazo ni Singida United, Yanga (zote kutoka Tanzania bara), Mlandege,  Jang’ombe Boys na Zimamoto (zote za visiwani Zanzibar).

Nao mabingwa watetezi wa kombe la mapinduzi , Azam FC walishindwa  kuendeleza wimbi la ushindi kwenye michuano hiyo baada ya kufungwa 1-0 na URA ya Uganda katika mchezo wa Kundi A . Azam FC ilimaliza pungufu baada ya winga wake Mghana, Enock Atta-Agyei kutolewa kwa kadi nyekundu.

Katika mchezo wa mwisho wa siku ya leo , klabu ya Yanga  imeendeleza ubabe katika michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Taifa ya Jang’ombe katika mchezo mwingine  wa Kundi B  uliopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar. Yanga nao wanapaa hadi nafasi ya pili wakiwa na  pointi tisa baada ya mechi tatu, sawa na vinara wa kundi hilo, Singida United ambao wapo juu kwa wastani mzuri zaidi wa mabao.

Siku ya kesho , Kutakua na mtanange mkali kati ya Simba SC na Azam FC saa 2:15 Usiku huku mechi hii ikitanguliwa na mchezo kati ya  Singida United  na JKU Saa 10:30 jioni .  Yanga itarudi uwanjani Jumapili kumenyana na Zimamoto FC.

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com