Yanga VS Ndanda FC hapatoshi leo…


Mabingwa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara , Yanga , leo watashuka dimbani uwanja wa Uhuru jijini Dar-es-salaam kuumana na klabu ya Ndanda FC .

Yanga ambao wanakamata nafasi ya 7 kwenye msimamo wa ligi , wakiwa na pointi 5 hadi sasa , historia inaonyesha katika mechi 6 walizowahi kukutana na Ndanda FC , Wameshinda mechi 2 , wamepoteza mechi moja na nyingine wametoka droo huku mechi zote wakishindia uwanja wa nyumbani  .

Yanga itaingia kwenye mchezo wa leo ikiwa na matumaini makubwa ya ushindi hasa baada ya taarifa kuwa tayari wamelipwa madeni ya mshahara wa miezi miwili waliyokua wanadai wachezaji na viongozi yanayokadiriwa kuwa ni shillingi milioni 238 .

Katika mchezo wa leo , Yanga watamkosa mshambuliaji wake , Mrundi Amissi Tambwe  ambaye amekuwa nje tangu mwanzoni mwa msimu akiuguza  maumivu yake ya goti, ambayo yalimuanza msimu uliopita na sasa yanaelekea kuwa sugu.

Nahonda wa Yanga , Thabani Kamusoko atarejea leo uwanjani huku safu ya ushambuliaji ya Yanga ikitegemewa kuongozwa na Donald Ngoma , Ibrahim Ajib na Obrey Chirwa .

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com