Yanga yaifunga Ndanda FC 1 – 0


Klabu ya Yanga leo imeweza kuutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani na kuibuka na ushindi wa goli 1 – 0 dhidi ya Ndanda FC katika mchezo wa raundi ya 4 ligi kuu ya vodacom Tanzania Bara .

Bao la pekee la Yanga lilifungwa na Ibrahim Ajib kwa kichwa dakika ya 36 baada ya kumalizia vizuri mpira uliopigwa na Kelvin Yondani.

Timu zote hazikucheza vizuri na kujikuta wachezaji wao wakipatamiana na kusababisha baadhi yao kulimwa kadi za njano.
Wachezaji walioonyeshwa kadi za njano ni Papy Shishimbi na Raphael Daud kwa upande wa Yanga na Jabir Aziz alionyeshwa kadi ya njano kwa upande wa Ndanda.

Kocha wa Ndanda , Malale Hamsin aliwaingiza Kelvin Friday na Ophen Fransis kuchukua nafasi za Rajab Zahir na Kapama ili kuongeza kasi katika idara ya ushambuliajj lakini walishindwa kubadili matokeo.

 

Yanga imefikisha pointi nane ambapo sasa imewakuta watani wao wajadi Simba ambao juzi Alhamisi ilibanwa mbavu na Mbao FC kwa kulazimishwa sare ya 2 – 2 .

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com