Yanga yashusha mshambuliaji mpya kutoka Swaziland..


Mabingwa wa ligi kuu Tanzania bara , klabu ya  Yanga inategemewa kumpokea mshambuliaji mpya   ,  Kabamba Tshishimbi kutoka Mbabane Swallows ya Swaziland.

Habari kutoka ndani ya Klabu ya Yanga zinaeleza kuwa tayari mazungumzo na mshambuliaji huyo yameshafika katika hatua nzuri na anatarajiwa kutua nchini siku yoyote kuanzia leo.

“Usajili bado unaendelea, tunataka kumpa kocha kila aina ya mchezaji aliyependekeza, lengo ni kuendelea kutetea ubingwa, uamuzi wake ndio utatufanya viongozi tufunge mchakato wa kusajili nyota wapya,” alisema kiongozi mmoja wa Yanga.

Aliongeza kuwa mchezaji huyo hahitaji kufanyiwa majaribio kutokana na kufuzu kupitia video zake na ni mwenye uzoefu na michuano ya kimataifa.

Usisahau kujisajili kwenye mchezo mpya wa ligi kuu Tanzania bara | BONYEZA HAPA KUJIUNGA .Tufuate facebook , twitter na instagram .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com