Yanga yasonga mbele ligi ya mabingwa Afrika…


Klabu ya Yanga leo jioni imefanikiwa kusonga mbele katika michuano ya kuwania kombe la mabingwa Afrika baada ya kutoka sare ya goli 1 – 1 dhidi ya  klabu ya  Saint Louis  katika mchezo wa marudiano wa Raundi ya Awali , mchezo uliopigwa katikaUwanja wa Linite mjini Victoria, Shelisheli.

Yanga ndio walikuwa wakwanza kupata bao kupitia kwa mshambuliaji wao Ibrahim Ajibu dakika ya 45 kipindi cha kwanza huku  Saint Louis wakipata bao la kusawazisha dakika ya 92 ya mchezo .

Kwa matokeo ya leo , Yanga wanasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 baada ya Februari 10 kuibuka na ushindi wa goli  1-0 , mchezo uliopigwa katika  Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Yanga kwasasa hawajajua watacheza na nani hatua inayofuata huku wakisubiri   mshindi kati ya Al-Merrikh Sc ya Sudan au Township Rollers ya Botswana mchezo ambao bado unaendelea .

Tufuate instagram , facebook na twitter .Unaweza pia kutuma stori yako ya michezo na sisi kuiweka kwa kubonyeza HAPA . Pia kutangaza nasi tutumie email , bongosoka@gmail.com